
Amani ndio utajiri wa thamani rohoni mwangu.
Sio pesa,sio umaarufu,bali utulivu wa moyo ndio hunifanya nisimame imara kila siku.
Katika dunia yenye kelele na presha nyingi,nimejifunza kuwa kulinda Amani yangu ya ndani ni uwekezaji muhimu kuliko wote. Amani hunipa clarity ya kufikiri,nguvu ya kusamehe,na hekima ya kuendelea mbele hata wakati wa mambo magumu.
Leo nikumbushe: usiuze Amani yako kwa chochote. Chagua utulivu, chagua shukrani,chagua upendo. Ndipo utajiri wa kweli utakaa moyoni mwako!